“Wajasiriamali kila muda huwa wana pitch” Strive Masiyiwa.
Ni nukuu ambayo ilichukua hatamu na kua chachu ya space yetu ya kwanza, kwenye STADIspace yetu ya kwanza.
Baadaye katika mapambano na kuitikia wito wa ujasiriamali nilikuja kugundua wajasiriamali makini hawaachi kuongelea biashara yao kwa watu mbali mbali”.
Hii inanifanya kuja kuamini “pitching” kuwa ujuzi wa lazima kwa wajasiriamali wengi wanao tamani mafanikio,hivyo hatuna budi bali kujifunza namna bora ya ku pitch
“Kama Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni yako mwenyewe, utatarajiwa kuwa muuzaji mkuu, kwa hivyo unatakiwa uwaonyeshe wawekezaji kuwa unajua jinsi ya kuwauzia kampuni yako mwenyewe” Caroline Cummings
Kabla ya yote tujiulize maana haswa ya “pitching”?
Je, inahusiana kwa namna moja ama nyingine na kufanya mauzo? tuseme salesmanship? au ni tofauti?
Haya yote ni maswali tuliyotarajia yatachochea mazungumzo yetu kwenye STADIspace.
Kabla ya jambo lolote, ikabiidi nimuulize Bw. Google mjuaji wa kila kitu
“Je kuna tofauti gani kati ya pitching na kufanya mauzo?
Kutokana na machache ya majibu kutoka Google ni kuwa haya maswala mawilli hayana tofauti kubwa lakini pia inategemea unamsikiliza nani mfano baadhi ya maoni
1“Kunaweza kuwa na fursa nyingi, ili kweza kuuza lakini kwenye“pitching” mara nyingi nafasi ni moja tu”
2“Pia tofauti na pitching ambayo inaweza kuwa fursa ya mara moja mauzo hujengwa kupitia mundelezo wa mahusiano ya kati ya mteja na wewe unaye fanya mauzo.
Unakubaliana na majibu ya Google…?
Tupe maoni yako?
Kama njia ya kuibua mazungumzo zaidi, tuliuliza hadhira ya Twitter kuhusu “ ni muda gani pitch inabiidi idumu?
Tulipata majibu mazuri huku wengi wakipendekeza pitching kufanywa kwa muda wa wastani wa dakika 3 hadi dakika 10 na ikibiidi hata hadi dakika 30 itakua sio mbaya.
Mwana jamvi mmoja kwa jina Goodluck alidokeza na kusema pitching inategemea kile unachoongelea na ambaye unamwambia “Baadhi ya pitching inaweza ikawa chini ya dakika 1”
Majibu ya tweet yalitoa muongozo wa maongezi kwenye Twitterspace yetu iliyofanyika baadaye jioni hio.Na yalikuja kua mazungumzo maridadi ambayo yalidumu kwa zaidi ya masaa 2.
Patrick ambaye wasifu wake wa Twitter unasomeka “pitchman I can help you sell it.
Alikuwa wa kwanza kushika hatamu na kusema kuwa siku zote mtu unatakiwa kuhakikisha watu wanaona kuwa unao uwezo wa kutoa kitu kuanzia kua wazo tu na kua bidha.
Pia uwe na uwezo wa kuendeleza zaidi hio biashara ili watu watakuamini na uwekezaji wao.
“Onesha upekee wako na ubora wako kwa sababu wewe ndo utakuja kuaminiwa kuendesha fursa hiyo”
Katika wazo hilohilo, Sume Rossmi ambaye ni mwanzilishi mwenza wa Naona Tv alisisitiza zaidi kuwa watu huwekeza kwa watu wanao wajua na sio kuwekeza kwenye mawazo pekee hivyo
“Jaribu kuthibitisha kwamba una uwezo kuliko mtu mwingine yeyote huko nje wa kutekeleza mawazo hayo”
Baadaye katika muendelezo wa mazungumzo
Faustine mwanzilishi wa Rednet company aligusia umuhimu wa kutafiti watu unaotaka uwavutie waje wawekeze katika wazo lako.
jaribu kujua vitu kama “historia yao kibishara na ni nyanja zipi huwa wanawekeza fedha zao, na pia maono yao ni yapi pamoja na matarajio yao’
Lazima uwafanyie utafiti watu unaokwenda ku pitch idea zako, je wana interest na lile wazo au biashara unayotaka kuwaelezea?”.
Hoja hii naihusisha na kile nilicho wahi kusikia na kujifunza nikiwa sehemu, STADI clinics mwaka 2022 ambapo Bw. Sameuel Nandala kutoka Deloitte pia alidokeza kuhusu umuhimu wa kufanya utafiti wa wafadhili kabla ya kuwafata,
“wakati mwingine taasisi za fedha hazikukopeshi si kwa sababu una biashara mbaya,bali kwa sababu tu hawakuelewa biashara unayofanya.Hivyo kama mjasiriamli jaribu kutafiti taasisi za fedha au mwekezaji yeyote kabla ya kwenda kutafuta ufadhili wowote kutoka kwao”
1. Kuhusiana na muda; pitch inapaswa kuwa ya muda gani?
Wengi wao walikubali kuwa hakuna kikomo sahihi cha muda maalum. Inaweza kua ya dakika 3 hadi 10. Yote inategemea tu ni nani unamuelekeza.
Hiyo ndo itaweza kuamua ni muda gani pitching inaweza kufanyika.
2. Ongelea zaidi kuhusu timu yako,
Jambo lingine la msimngi ni kwamba wakati wa pitching usizingatie sana wazo lako na kusahau kuwaelezea watu watakaao paswa kuhakikisha hili wazo linakuja kuiona kesho.
Hawa ndio watu ambao watafanya mipango yote itimie, sasa kwa nini usiwazingatie zaidi.Ikiwezakana zaidi elezea zaidi utaalamu wao,mmefanya nini hapo nyuma.
shauku, na kujitolea kwa kile unachojenga.
Thibitisha kuwa wewe una timu inayoweza kutimiza kile kitu ambacho umeahidi.
inasemekana Wawekezaji wengi wako tayari kuwekeza katika timu “A” (an A team) team yenye wazo la wastani kuliko timu “B” yenye wazo la wastani.
Kitu ninachopata pia kutoka kwa maonyesho na mashindano ninayotazama.
Daima wanajaribu kuelezea kuwa kwamba hawapo kwa ajili ya pesa tu.
Bali ni zaidi kuhusu maono na athari chanya unayoahidi kuleta kwa jamii. Ni watu gani hao wa kuleta wazo hili kwenye maisha haya ya kawaida
Thibitisha kuwa wewe una timu inayoweza kutimiza kile kitu ambacho umeahidi.
inasemekana Wawekezaji wengi wako tayari kuwekeza katika timu “A” an a team yenye wazo la wastani kuliko timu “B” yenye wazo la wastani.
3.Koleza pitch yako kwa kutumia hadithi
Kama msemo wa kawaida unavyosema, “hadithi nzuri inakuvuta ndani,laki hadithi bora humuweka muwekezaji katika viatu vyako.
Kuambatanisha pith yako na simulizi nzuri huonesha kuwepo kwa uhusiano wa moja kwa moja kati yako wewe na fursa unayo jaribu kuitatua.
Lakini pia endelea kuhusisha simulizi yako na watu unaojaribu kufanya pitching kwao.
4. Tumia data na takwimu kuelezea hadithi yako.
Baada ya kuwa na simulizi nzuri kuhusu biashara basi hakikisha unaimbatanisha na ushahidi wa takwimu hesabu nyinmgine
Kama msemo maarufu unaosema “Namba hazidanganyi”,kwa hiyo ikiwa una takwimu zinazo weza kutetea unacho kiongelea itakuwa viziri zaidi.
Takwimu husaidia
mfano mpaka sasa
umepata wateja wangapi?Vipi kuhusu mauzo?
Je,mwenendo wa uchumi unasemaje? Ni vizuri kuzijumuisha hivi kwa
Je kutokana na mazingira ya kiuchumi ina favour biashara yako?
Mwisho kabisa ntazitaja hoja zingine zilitolewa kwenye kile kinachofanya pitch kuwa nzuri:
5.Jiamini.
6. Jifunze zaidi kama njia ya kuboresha pitch yako
7. Tarajia maswali kutoka kwa hadhira au kutoka kwa wawekezaji na jiulize utayajibu vipi
8. Usitumie takwimu za uongo.